Flo Rida ‘My House’ imenifikia na video yake ninayo hapa tayari. (Video).

Baada ya kuachia GDFR, rapper kutoka Miami, Marekani Flo Rida ameamua kurudi na video ya wimbo wa My House, wimbo unaopatikana kwenye EP yake aliotoa miezi michache iliyopita.
Kama wewe ni shabiki wa Flo Rida basi video hii ikufikie kokote uliko mtu wangu, My House ni moja ya zile nyimbo ambazo zitakufaya uinuke na ucheze popote pale ulipo… video yake ninayo hapa chini tayari, karibu uitazame.