@GoodNews single ya Belle 9; ‘Shauri zao’ imepata nafasi ya kuonekana kwenye Trace Urban!
Inafurahisha kuona muziki wa Tanzania ukiwakilishwa vizuri na wasanii wetu, wasanii wengi siku hizi wanapigania kupeleka muziki wa Bongo Fleva kwenye soko la kimataifa na jitihada za wasanii wetu kwenda kimataifa zinaonekana pale ambapo vituo vya kimataifa kama TRACE na MTVBase Africa kupiga nyimbo za wasanii kutoka Tanzania!
Kama wewe ni shabiki wa Belle 9 basi hii good news ikufikie popote ulipo ndugu yangu, single mpya ya msanii huyo “Shauri zao” imechezwa leo kwenye kituo kikubwa cha kimataifa Africa, Trace Urban kwenye segment yao ya “Brand New”.
Kuonyesha furaha yake, Belle 9 alipost hii picha kupitia page yake ya Instagram, na caption ya maneno iliyosema…
>>>“Much respect and big time appreciation for ur support, our utmost gratitude goes out to the whole trace network @trace_urban @tracenigeria”… “ <<< @belle9tz.
Nimekusogezea video ya Belle 9 hapa chini, video imetengenezwa hapa hapa Tanzaniachini ya Director wa hapa hapa nyumbani, Hanscana.