China yatakiwa kusitisha ujenzi baharini
Uwanja wa ndege unaojengwa na China katika visiwa vya Spatry
Marekani imetaka kuwepo usitishwaji wa ujenzi wa miradi kwenye maeneo yanayozozaniwa katika bahari ya kusini mwa China.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter aliuambia mkutano mkuu wa ulinzi nchini Singapore kuwa tabia ya China eneo hilio imekiuka sheria za kimataifa Carter amesema kuwa kuvihami kijeshi visiwa bandia ambavyo vinajengwa na China ni hatua inayoweza kusababisha mizozo ya kijeshi. Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya makao makuu ya jeshi la marekani kusema kuwa china imeweka silaha katika moja ya visiwa hivyo. Bwana Carter anasema kuwa hakutakuwa na suluhu la kijeshi . Hata hivyo amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa na jeshi lake katika eneo hilo.
No comments